List Headline Image
Updated by Kumjua Mwenyezi Mungu Lee on Oct 18, 2019
Headline for Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee
 REPORT
163 items   11 followers   2 votes   1.03k views

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu wanaomilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.

Swahili Christian Praise Song "Anga Hapa ni Samawati Sana"

**Swahili nyimbo za dini "Anga Hapa ni Samawati Sana"

**

I

Aa ... hii hapa anga,

oh ... anga iliyo tofauti sana!

Harufu ya kupendeza inasambazwa kote kwenye nchi, na hewa ni safi.

Mwenyezi Mungu alikuwa mwili na anaishi miongoni mwetu,

Akionyesha ukweli na kuanza hukumu ya siku za mwisho.

Maneno ya Mungu yanaweka wazi ukweli wa upotovu wetu,

tunatakaswa na kukamilishwa na kila aina ya jaribio na usafishaji.

Tunayaaga maisha yetu maovu na kubadilisha sura yetu ya zamani kuwa sura mpya.

Tunatenda na kuzungumza kwa maadili na kuruhusu maneno ya Mungu yatawale.

Moto wa upendo wetu kwa Mungu unawashwa mioyoni mwetu.

Tunasambaza maneno ya Mungu, kumshuhudia, na kusambaza injili ya ufalme.

Tunajitolea nafsi yetu yote kumridhisha Mungu, na tuko tayari kuteseka maumivu yoyote.

Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu kwa kubadilisha jaala yetu.

Tunaishi maisha mapya na tunakaribisha kesho mpya kabisa!

II

Ndugu wanapokutana pamoja, furaha inaonyesha kwenye nyuso zao.

Tunasoma maneno ya Mungu na kushirikiana ukweli, tunaungana katika upendo wa Mungu.

Sisi ni watu waaminifu, safi na wazi, hakuna ubaguzi kati yetu.

Tunaishi kwa ukweli, tukipendana, tukijifunza kutoka kwa nguvu za kila mmoja na kurekebisha upungufu wetu.

Kwa akili moja tunatimiza wajibu wetu na kutoa dhabihu yetu.

Katika njia ya kwenda katika ufalme, maneno ya Mungu hutuongoza kupita dhiki na taabu.

Maneno ya Mungu hufunua uweza Wake, na hushinda na kufanya kundi la washindi.

Wateule wa Mungu kutoka katika mataifa yote wanarudi mbele ya Mungu.

Watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu na kumwabudu milele.

Mapenzi ya Mungu yanatendwa duniani, ufalme wa Kristo umeonekana.

Haki na utakatifu wa Mungu vinadhihirika, mbingu na dunia zinafanywa upya.

Watu wa ufalme wanamwogopa Mungu na kuepuka mabaya, na wanaishi katika nuru.

Watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu na kumwabudu milele.

Mapenzi ya Mungu yanatendwa duniani, ufalme wa Kristo umeonekana.

Haki na utakatifu wa Mungu vinadhihirika, mbingu na dunia zinafanywa upya.

Watu wa ufalme wanamwogopa Mungu na kuepuka mabaya, na wanaishi katika nuru.

Ee, we … hii ni anga,

oh ... anga iliyo tofauti sana!

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi" | The True Love of God for Man

**Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi" | The True Love of God for Man

**
Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000,
uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi.
Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme ni awamu ya mwisho.
Ingawa kazi ya Mungu ni tofauti katika kila moja,
yote inalingana na kile ambacho binadamu wanahitaji,
ama hasa inalingana na ujanja ambao Shetani anatumia, anapopigana na Yeye.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.

Ni ili kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua upotovu mbaya wa Shetani,
kufunza viumbe kutofautisha mema na mabaya,
na kumjua Mtawala wa vitu vyote ni Mungu Mwenyewe.
Kuona wazi kuwa Shetani ni adui wa mwanadamu, kuwa ni yule mwovu, mhalifu,
ili mwanadamu aweze kutofautisha mema na maovu, ukweli na uongo,
utakatifu na uchafu, na makuu kutoka kwa ya chini.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.
Kumfanya binadamu pumbavu kuwa na ushuhuda Kwake:
Sio Mungu ndiye Alileta upotovu wa mwanadamu,
na ni Mungu Mwenyewe pekee, Bwana wa uumbaji,
Anayeweza kuweka vitu vya kufurahia na kumletea mwanadamu wokovu.
Hii ni ili waweze kujua kuwa Mungu ni Mtawala wa vitu vyote,
kuwa Shetani ni uumbaji Wake, ambaye baadae alichagua kumgeuka.

Mpango wa Mungu wa miaka 6,000 wa usimamizi umegawanywa katika hatua tatu,
ili yafuatayo yaweze kufikiwa:
kuruhusu viumbe Wake kuwa mashahidi Wake,
kujua mapenzi Yake, na kuona kuwa ukweli ni Yeye.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Tufuate: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

**Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

**

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.

Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.

Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.

Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.

Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.

Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia.

Tunaondolewa vizuizi na ubaguzi wetu, tunaishi ndani ya upendo wa Mungu.

Tunaelewa ukweli na kuwekwa huru, mioyo yetu ni tamu kama asali.

Tunapendana, hakuna umbali kati yetu.

Tunaelewa moyo wa Mungu, sisi si hasi tena.

Tukiishi ndani ya maneno ya Mungu, tunaona uzuri Wake.

Tumechukua njia ya nuru maishani, haya yote ni mwongozo wa Mungu.

Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha.

Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu.

Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani.

Maneno ya Mungu ni yenye thamani sana, yote ni ukweli kabisa.

Tunapokubali hukumu ya maneno ya Mungu, upotovu wetu unafunuliwa kabisa.

Kwa tabia fidhuli, tunakosa mantiki kweli.

Maneno ya Mungu hutupogoa na kutushughulikia, tumekuja kujijua wenyewe.

Tunajitafakaria, kujielewa, na kuwa na toba ya kweli.

Kupitia hukumu na kuadibu, upotovu wetu unatakaswa.

Tunatupa tabia zetu potovu, tunakuwa wanadamu wapya.

Tunaweza kutekeleza wajibu wetu vizuri kulipa upendo wa Mungu.

Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake, tunajitolea kwa Mungu.

Tunasimama imara katika ushuhuda kutimiza mapenzi ya Mungu.

Kila mmoja anatoa mwanga wake mwenyewe, mwali wake mwenyewe, kumtangaza na kumshuhudia Mungu.

Upendo safi na aminifu kwa Mungu ni wenye furaha na mtamu.

Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha.

Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu.

Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani.

Sisi huunga mioyo na mikono kushuhudia kwa Mungu.

Tunaeneza injili ya ufalme, tusiogope kamwe ugumu au uchovu.

Katika mateso na majaribu, tunamwomba na kumtegemea Mungu.

Njia ni yenye mabonde na milima, lakini Mungu hufungua njia.

Tunapoelewa ukweli wa maneno ya Mungu, mioyo yetu hupata nguvu.

Maneno ya Mungu yanatuhimiza, tunazidi kwenda mbele milele.

Sako kwa bako, mkono kwa mkono tunamshuhudia Mungu, tunajitoa Kwake mwili na akili.

Haijalishi ukubwa wa mateso yetu, tuko tayari sana.

Kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, tunamshinda Shetani.

Tunampenda Mungu kweli, hatutajua kamwe.

Tumeliacha kabisa joka kuu jekundu, sisi ni askari washindi.

Tunashuhudia katika njia yetu ya upendo kwa Mungu, hatutarudi nyuma kamwe.

Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha.

Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu.

Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani.

Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha.

Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu.

Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

**Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

**
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili. Kama kusingekuwa na udhibiti na ukuu wa Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kudumisha na kuweka wiano katika mazingira, hata kama yaliumbwa na Mungu kwanza.”

Swahili Christian Song "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu" | The Lord Has Come Back (Tai Chi Dance)

**nyimbo za injili "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu" | The Lord Has Come Back (Tai Chi Dance) Kuonekana kwa Mungu kunataja kufika Kwake binafsi duniani il...

**
Swahili Christian Song "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu" | The Lord Has Come Back (Tai Chi Dance) Kuonekana kwa Mungu kunataja kufika Kwake binafsi duniani ili kufanya kazi Yake. Na utambulisho Wake mwenyewe na tabia, na kwa njia Yake mwenyewe, Yeye anashuka kati ya mwanadamu ili kuanza enzi na kumaliza enzi. Kuonekana kama huku sio ishara ama picha. Si aina ya sherehe. Si muujiza. Si ono kuu. Pia sio aina ya mchakato wa kidini hata zaidi. Ni ukweli halisi ambao unaweza kuguswa na kuonwa, ukweli ambao unaweza kuguswa na kuonwa. Konekana kama huku sio kwa ajili ya kufuata mchakato, ama kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; lakini ni, kwa ajili ya hatua ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu. Kuonekana kwa Mungu kila mara ni kwa maana, na kuna uhusiano na mpango Wake wa usimamizi, kuna uhusiano na mpango Wake wa usimamizi.Konekana huku si sawa kabisa na kuonekana kwa Mungu akiongoza mwanadamu, kumwongoza mwanadamu au kumtia nuru mwanadamu, kumwongoza mwanadamu au kumtia nuru mwanadamu. Mungu anafanya hatua ya kazi kuu kila wakati Anapojifichua Mwenyewe. Kazi hii ni tofauti na ile ya enzi nyingine yoyote, isiyoweza kufikiriwa na mwanadamu, haijapitiwa na mwanadamu kamwe, haijapitiwa na mwanadamu kamwe. Ni kazi inayoanzisha enzi mpya na kumaliza enzi nzee, kazi mpya na bora ya wokovu wa binadamu, na kazi ya kumleta binadamu katika enzi mpya. Ni umuhimu wa kuonekana kwa Mungu. kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana. Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake.Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii. Maudhui ya video hii yametafsiriwa yote na wafasiri wataalam. Hata hivyo, kutokana na tofauti za lugha nk, makosa kadhaa yaliyofanywa hayawezi kuepukika. Ukigundua makosa yoyote kama hayo, tafadhali rejea kwa toleo la kwanza la Kichina. Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. IInjili ya Kushuka kwa Ufalme:Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. IInjili ya Kushuka kwa Ufalme:Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi.

Wimbo Mpya wa Dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu"

**wimbo wa dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Have You Enjoyed the Joy of Gaining the Work of the Holy Spirit? (Official Video)

**
Wakati hamumwelewi Mungu na hamjui asili Yake,

mioyo yenu haiwezi kamwe kufunguka, kufungukia Mungu.

Mara utakapomwelewa Mungu wako, utaelewa kilicho moyoni Mwake,

na kufurahia kilicho ndani Yake kwa imani na usikivu wako wote.

Unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, kidogo kidogo, siku baada ya siku,

unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utakuwa wazi Kwake.

Moyo wako unapokuwa wazi kweli, moyo wako unapokuwa wazi kweli,

utaiona dharau, utaiona aibu

ya maombi yako ya kupita kiasi na yenye ubinafsi.

Moyo wako unapokuwa wazi kweli,

moyo wako unapokuwa wazi kweli,

utaona dunia isiyo na mwisho moyoni mwa Mungu,

na kuwa katika ulimwengu wa maajabu yasiyosimuliwa.

Hakuna giza mabaya au uongo,

Unapoufungua Moyo wako kwa Mungu.

Ni ukweli tu, imani tu mwanga tu haki kote.

Unapoufungua Moyo wako kwa Mungu.

Yeye ni upendo, Yeye anajali, ana huruma isiyo na mwisho.

Maishani mwako, unahisi furaha,

Unapoufungua moyo wako kwa Mungu.

Hekima na nguvu Zake zinajaza ulimwengu huu,

vile vile mamlaka na upendo Wake.

Unaweza kuona kile Mungu anacho na Alicho

Kinachomletea furaha, na kinachomletea matatizo,

kinachomletea huzuni na hasira, vyote viko wazi kwa wote kuona,

unapoufungua moyo wako kwa Mungu na kumwalika aingie ndani.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

6

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

**Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

**
Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Wanadamu walikuwa wapotovu sana, walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanatunzwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa waasherati kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko wa kutisha. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo zaidi, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.

Kisha angalia enzi ya sasa: Hawa watu wenye haki kama Nuhu, ambao wangeweza kumwabudu Mungu na kuepuka uovu, wamekoma kuwepo. Lakini bado Mungu ana fadhili kwa mwanadamu huyu, na Anamsamehe mwanadamu wakati huu wa enzi ya mwisho. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake. Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi ya binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumvulia mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.

Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.

Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo, bila kujulikana kwa mwanadamu, majaliwa ya nchi yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kwa hiyvo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.

Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.

Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.

Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.

Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.

Chanzo: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

**Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu” Mwenyezi Mungu anasema, “

**
Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanya kazi na pamoja na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao. Wawe ni manabii au binadamu wanaotumiwa na Mungu kutoka kwa enzi zilizopita, hakuna yeyote anayeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.” “Kwani kiini cha binadamu ni tofauti na kile cha Mungu. Binadamu hawezi kamwe kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, sembuse kuwa Mungu. Kile ambacho Roho Mtakatifu anamwelekeza binadamu kuishi kwa kudhihirisha ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu.”

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili

**Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili

**
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. ... Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.”

Tufuate: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

9

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

**Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

**
Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewazia hili: Mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia kufika kwa wakati huo, na uaminifu wenu ni wa kusifika, imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: Wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi? Iwapo ninyi ni wa kwanza kati ya wale ambao Yesu Atawashukia, Je, wengine hawataona jambo hili kama lisilo la haki sana? Najua kuwa nyinyi mna ukweli mkubwa na utiifu kwa Yesu, lakini mmewahi kukutana na Yesu? Mnajua tabia Yake? Mmewahi kuishi na Yeye? Mnaelewa kiasi gani kumhusu kwa kweli? Wengine watasema kuwa maneno haya yanawaweka katika tatizo gumu. Watasema, “Nimesoma Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho mara nyingi sana. Nitakosaje kumwelewa Yesu? Usijali kuhusu tabia ya Yesu—najua hata rangi ya nguo Alizopenda kuvaa. Je, haushushi hadhi yangu ukisema simwelewi?” Napendekeza kuwa usiyapinge masuala haya; ni heri utulie na kufanya ushirika juu ya maswali yafuatayo: Kwanza, unajua uhalisi ni nini, na nadharia ni nini? Pili, unajua dhana ni nini, na ukweli ni nini? Tatu, unajua kile kinachowazwa na kile kilicho halisi?

Watu wengine wanakataa ukweli kuwa hawamwelewi Yesu. Ilhali Nasema hammwelewi hata kidogo, na hamwelewi hata neno moja la Yesu. Hiyo ni kwa sababu kila mmoja wenu anamfuata Yeye kwa sababu ya matukio ya Biblia, kwa sababu ya yale yaliyosemwa na wengine. Hamjawahi kumwona Yesu, sembuse kuishi na Yeye, na hata hamjapata kushinda na Yeye hata kwa muda mfupi. Hivyo, je, kuelewa kwenu kuhusu Yesu sio nadharia pekee? Je, si kuelewa kwenu kunakosa uhakika? Labda watu wengine wameiona picha ya Yesu, ama wengine wametembea nyumbani kwa Yesu kibinafsi. Labda wengine wamegusa mavazi ya Yesu. Ilhali kuelewa kwako kumhusu bado ni kwa nadharia na ila si kwa vitendo, hata kama umeonja chakula kilicholiwa na Yesu binafsi. Haijalishi ni hali ipi, hujawahi kumwona Yesu, na hujawahi kuwa pamoja na Yeye katika hali ya kimwili, na hivyo, kuelewa kwako kumhusu Yesu kutabaki kuwa nadharia tupu daima ambako hakuna ukweli. Pengine maneno Yangu yana uvutio mdogo kwako, lakini Nakuuliza hivi: Ingawa labda umesoma maandishi mengi yaliyoandikwa na mwandishi unayempenda, je, unaweza kumwelewa kikamilifu bila kuwahi kukaa na yeye kwa muda? Je, unajua tabia yake ilivyo? Je, unajua ni maisha ya aina gani anayoishi? Unajua chochote kuhusu hali ya hisia zake? Huwezi hata kumwelewa kikamilifu mwanadamu unayempenda, sasa utawezaje kumwelewa Yesu Kristo? Kila kitu unachoelewa kumhusu Yesu kimejaa mawazo na dhana, na hakina ukweli wowote wala uhalisi. Kinanuka, na kimejaa mwili. Kuelewa kwa aina hii kutakuwezesha vipi kustahili kukaribisha kurejea kwa Yesu? Yesu hatawakaribisha wale waliojawa na mawazo na dhana za mwili. Wale wasiomwelewa watafaa vipi kuwa waumini Wake?

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeidaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Utaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Chanzo: Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Upendo wa Mungu na wokovu | "Kutanafusi kwa Mwenye Uweza" Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

**Upendo wa Mungu na wokovu | "Kutanafusi kwa Mwenye Uweza" Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kuchunguza, kuuchunguza moyo na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuamsha, ili usipate kiu na kupata njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote."

Tazama Video: Sauti ya Mungu

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?"

**Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?"

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyoongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa kwa binadamu, na tofauti kwamba mmoja anachukuliwa katika mimba na Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike."

Neno la Mungu | "Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu"

**Neno la Mungu | "Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu"

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Yeye ambaye Anafanya kazi katika Uungu Anawakilisha Mungu, ilhali wale wanaofanya kazi katika ubinadamu ni wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Yaani, Mungu katika mwili ana utofauti halisi na wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya Uungu, lakini wanadamu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu anaongea binafsi kuzindua enzi mpya na kuleta mwanadamu kwenye mwanzo mpya. Wakati Yeye Atamaliza mazungumzo Yake, itaashiria kwamba kazi ya Mungu katika Uungu imekamilika. Baada ya hapo, wanadamu wote hufuata mwongozo wa wale hutumiwa na Mungu kuingia katika uzoefu wa maisha. Vile vile, katika hatua hii Mungu huleta mwanadamu katika enzi mpya na Anampa kila mwanadamu mwanzo mpya. Na hivyo, kazi ya Mungu katika mwili inahitimishwa."

Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"

**Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"

**
Mungu alikuja duniani hasa kutimiza ukweli wa "Neno kuwa mwili."
(tofauti na Agano la Kale, katika siku za Musa,
Mungu alizingumza moja kwa moja kutoka mbinguni).
Kisha, yote yatatimizwa katika enzi ya Ufalme wa Milenia
kuwa ukweli ambao watu wanaweza kuona,
ili watu waweze kuona utimizaji hasa kwa macho yao wenyewe.
Hii ni maana ya kina ya Mungu kuwa mwili.
Yaani, kazi ya Roho imekamilika kupitia kwa mwili na neno.
Hii ni maana ya kweli ya "Neno kuwa mwili, Neno kuonekana katika mwili."
II
Ni Mungu tu Anayeweza kuzungumza mawazo ya Roho,
na ni Mungu tu katika mwili anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho.
Neno la Mungu linaonekana katika Mungu aliyepata mwili.
Mtu yeyote yule ataongozwa na hili,
hakuna anayeweza kuzidi hili na kila mtu anaishi ndani ya mipaka hii.
Kutokana na tamko hili watu watapata ufahamu;
isipokuwa kupitia haya matamshi hakuna atakayeota kuhusu kupokea
tamko kutoka mbinguni.
Haya ni mamlaka ambayo yameonyeshwa na Mungu kuwa mwili,
ili kila mtu ashawishike.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Sikiliza nyimbo: nyimbo za kusifu

Wimbo wa Injili 2018 | "Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu"

**Wimbo wa Injili 2018 | "Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu"

**
Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu,
na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake.
Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho.
Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu,
kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.
II
Mungu amekanyaga vitu vyote na miguu Yake,
Yeye ananyosha mtazamo Wake juu ya ulimwengu.
Na Mungu ametembea kati ya wanadamu,
ameonja utamu na uchungu, ladha zote za dunia ya mwanadamu;
lakini wanadamu, kamwe hawakumtambua Mungu kweli,
wala hawakumwona Mungu alipokuwa akitembea ughaibuni.
Kwa sababu Mungu alikuwa kimya, na hakufanya matendo yasiyo ya kawaida,
hivyo, hakuna aliyemwona kweli.
Vitu haviko vilivyokuwa awali:
Mungu anaenda kufanya vitu ambavyo, katika enzi zote, ulimwengu haujawahi kuona,
Mungu anaenda kunena maneno ambayo, katika enzi zote, wanadamu hawajawahi kusikia,
kwa sababu Yeye anawataka binadamu wote waje kumjua Mungu katika mwili.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi" | The True Love of God for Man

**Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi" | The True Love of God for Man

**
Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000,
uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi.
Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme ni awamu ya mwisho.
Ingawa kazi ya Mungu ni tofauti katika kila moja,
yote inalingana na kile ambacho binadamu wanahitaji,
ama hasa inalingana na ujanja ambao Shetani anatumia, anapopigana na Yeye.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.

Ni ili kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua upotovu mbaya wa Shetani,
kufunza viumbe kutofautisha mema na mabaya,
na kumjua Mtawala wa vitu vyote ni Mungu Mwenyewe.
Kuona wazi kuwa Shetani ni adui wa mwanadamu, kuwa ni yule mwovu, mhalifu,
ili mwanadamu aweze kutofautisha mema na maovu, ukweli na uongo,
utakatifu na uchafu, na makuu kutoka kwa ya chini.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.
Kumfanya binadamu pumbavu kuwa na ushuhuda Kwake:
Sio Mungu ndiye Alileta upotovu wa mwanadamu,
na ni Mungu Mwenyewe pekee, Bwana wa uumbaji,
Anayeweza kuweka vitu vya kufurahia na kumletea mwanadamu wokovu.
Hii ni ili waweze kujua kuwa Mungu ni Mtawala wa vitu vyote,
kuwa Shetani ni uumbaji Wake, ambaye baadae alichagua kumgeuka.

Mpango wa Mungu wa miaka 6,000 wa usimamizi umegawanywa katika hatua tatu,
ili yafuatayo yaweze kufikiwa:
kuruhusu viumbe Wake kuwa mashahidi Wake,
kujua mapenzi Yake, na kuona kuwa ukweli ni Yeye.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs

**Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs

**
Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo,
na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu.
Si kupita kiasi kusema hivyo,
kwani Ana kiini cha Mungu, Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake,
ambayo haifikiwi na mwanadamu.
Wale wanaojiita Kristo wenyewe ilhali hawawezi kufanya kazi ya Mungu ni wadanganyifu.
Wanaojifanya kuwa Kristo hatimaye wataanguka,
ingawaje wanadai kuwa Kristo,
hawana kiini chochote cha Kristo.

Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani,
lakini mwili hasa uliochukuliwa na Mungu.
Anapotekeleza na kutimiza kazi Yake kati ya mwanadamu.
Mwili huu hauwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote tu.
Ila mwili unaoweza kutosha kubeba kazi ya Mungu duniani.
Na kuonyesha tabia ya Mungu,
na kumwakilisha Mungu vizuri na kumpa mwanadamu uzima.
Hivyo Mungu anasema kuwa uhalali wa Kristo, hauwezi kufafanuliwa na mwanadamu,
lakini unajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
Hivyo kama kwa kweli unataka kutafuta njia ya uzima,
lazima kwanza utambue, ni katika siku za mwisho ambapo Anakuja duniani,
kumpa mwanadamu njia ya uzima.
Sio zamani, sio zamani; inafanyika leo.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu

**Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu

**
Upendo na huruma za Mungu
hupenyeza kazi Yake
ya usimamizi kwa utondoti.
I
Ikiwa mwanadamu ahisi mapenzi Yake ya huruma au la,
Yeye hachoki kufuatilia kazi Anayohitaji kufanya.
Ikiwa mwanadamu aelewa usimamizi Wake au la,
kazi Yake huleta usaidizi na utoaji unaoweza kuhisiwa na wote.
Upendo na huruma za Mungu
hupenyeza kazi Yake
ya usimamizi kwa utondoti.
II
Pengine leo huhisi upendo na uzima Mungu anaokupa,
mradi tu huondoki katika upande Wake,
wala kuachilia mapenzi yako ya kutafuta ukweli,
hakika siku moja utaiona tabasamu ya Mungu.
Sababu kusudi la Mungu katika kazi Yake ya usimamizi
ni kumpokonya mwanadamu kutoka milki ya shetani
na sio kuwaacha waliopotoshwa na Shetani,
na kupinga mapenzi Yake.
Upendo na huruma za Mungu
hupenyeza kazi Yake
ya usimamizi kwa utondoti.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Tazama Video:
Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video)

Maudhui Yanayohusiana:
Wimbo Mpya wa Dini | "Mungu Anapata Mwili ili tu Kumshinda Shetani na Kuwaokoa Binadamu"

Muziki wa Injili "Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele"

**Muziki wa Injili "Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele"

**
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Thamani na maana ya maneno Yake yanaamuliwa na kiini chao,
sio kama mwanadamu anayakubali au kuyatambua.
Hata kama hakuna mwanadamu ulimwenguni anayapokea maneno Yake,
thamani yao na usaidizi kwa mwanadamu hayapimiki.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.

Kwa wale wanaoasi, kupinga na kutoheshimu maneno Yake,
Jibu pekee la Mungu kwao ni hili:
Acha muda na ukweli uwe shahidi Wake,
uonyeshe maneno Yake ni ukweli, njia na uzima;
uonyeshe kuwa yote Aliyosema ni kweli,
ni kile ambacho mwanadamu anafaa kuwa nacho na kufuata.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.

Kwa wale wote wanaomfuata Mungu atawaruhusu kuona ukweli huu:
Wale ambao hawakubali maneno Yake au kuyatekeleza katika matendo yao,
na wale ambao hawawezi kugundua kusudi ama wanaokosa kupata wokovu katika maneno Yake,
Hawa wote ni wale watu ambao maneno ya Mungu yamewalaani.
Wamepoteza wokovu wa Mungu.
Kutoka kwao, adhabu Yake haitapotea mbali
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotazamwa Mara Nyingi: Wimbo wa Injili | Mungu Hutumaini Mtu Anaweza Kumjua na Kumwelewa | Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu

Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

**Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu."

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)

**Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi Yake, na maneno sasa yameelekezwa kwa watu wa ulimwengu mzima. Hii tayari ni nusu ya kazi. Roho wa Mungu amefanya kazi kubwa hiyo tangu dunia ilipoumbwa; Amefanya kazi tofauti katika enzi tofautitofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu, pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia kumwokoa mwanadamu aliyepotoka. Na siku hii, pia Anaweza kumshinda mwanadamu ambaye hamjui na kumfanya awe chini ya utawala Wake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishoni, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo si ya haki ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, wema, hekima, maajabu na utakatifu pekee, bali pia ni Mungu anayemhukumu mwanadamu."

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini"

**Maneno ya Roho Mtakatifu | "Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini"

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Katika nyakati zilizopita, watu wengi walifuatilia kwa jitihada na fikira za mwanadamu na kwa ajili ya matumaini ya mwanadamu. Mambo haya hayatajadiliwa sasa. La muhimu ni kupata njia ya kutenda ambayo itawezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele ya Mungu na hatimaye kuvunja pingu za ushawishi wa Shetani, ili mpate kuwa wakubalika wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha duniani matakwa ya Mungu kwenu. Ni haya tu yanayoweza kutimiza mapenzi ya Mungu."

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

**Neno la Mungu | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu."

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?"

**Maneno yaRoho Mtakatifu | "Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?"

**
Mwenyezi Mungu anasema, "Mnamtamani na kumcha tu Mungu msiyemwona aliye mbinguni lakini hauna haja na Kristo Anayeishi duniani. Hii pia si ni ukosefu wa imani? Mnamtamani tu Mungu Aliyefanya kazi kitambo kile lakini hutaki kukumbana na Kristo wa leo. Hizi ndizo huwa 'imani' zilizochanganyika katika mioyo yenu isiyomwamini Kristo wa leo. Sikuchukulii kwa hali ya chini kwa maana ndani yako mna kutoamini kwingi, ndani yenu mna uchafu mwingi sana ambao lazima uchunguzwe kwa kina. Madoa na uchafu huu ni ishara kuwa huna imani hata kidogo; ni alama za ukanusho wenu wa Kristo na huonyesha kuwa nyinyi ni msaliti wa Kristo. Hiyo ni kama kitambaa kinachofunika ufahamu wenu wa Kristo, kizuizi cha nyinyi kupatwa na Kristo, kitu kinachowakinga kulingana na Kristo, na dhihirisho kuwa Kristo Hawatambui."

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuijua Kazi ya Mungu Leo"

oho ### *Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuijua Kazi ya Mungu Leo"
*

Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho."

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.